Siri nzito inayomfanya Ali Kiba kuzidi kupendwa zadi na Bongo




Wasanii wengi wa fani mbali mbali kuanzia filamu hadi bongo fleva, wamekuwa wakipoteza mashabiki wao wengi kutokana na ile hali tu ya jinsi anavyochukulia umaarufu wake, kama anatumia umaarufu wake vizuri basi hutokea kupendwa sana na watu hata wale ambao siyo mashabiki wake, watampenda tu kama mtu wakawaida.Kismati hiki cha kupendwa sana na watu wa rika mbalimbali anacho naye msanii mkongwe sana Ali Kiba.



Ukimuongelea Msanii kama Ali Kiba, watu wengi wanatamani wasanii wote wawe kama yeye,ni mmoja kati ya wasanii wachache sana maarufu ambao hawana ulimbukeni wa mali au umaarufu wao, cause wengi wao pale wapatapo umaarufu kidogo tu, huanza kudharau watu wake wa karibu, haswa wakipata mali kidogo basi huishia kuonyesha watu magari na nyumba,hata kama haiwahusu, ilimradi tu basi nao waonekane kama wasanii wa nje wenye mali zao, ila kwa Ali kiba imekuwa ni tofauti sana,na hiki ndicho kinachofanya AliKiba aweze kupendwa zaidi na kila mtu.

Kupitia mtandao wa instagram Ali kiba aliweza kuweka wazi mtazamo wake wa mafanikio:

“Kuishi maisha halisi yenye furaha na maana kwako ni kitu cha thamani sana. Unayo kila sababu ya kufuata njia yako ya maisha yenye misingi mizuri ya kukujenga katika kila nyanja ya maisha yako. Kwa kuwa kila mtu ana maono yake binafsi kuhusu maisha ni vigumu kufafanua maana halisi ya maisha. Naamini nawe pia una falsafa yako ya kutafsiri nini maana ya maisha mazuri kwako,”



“ 1. Kuwa mkweli kwako mwenyewe. -Maisha mazuri hutafsirika na mtu mwenyewe, labda mimi naweza kukuambia maisha mazuri kwangu ni kuwa mwenye furaha na familia yangu, mpenz wng afya njema, kijana mtanashati, hodari na mwenye kujitegemea mwenyewe. Nawe pia una maono yako labda ni tofauti na yangu, ni hayo maono yako ndiyo yanayokutambulisha na kukufanya uishi kwa misingi uliyojiwekea. “

“Faraja katika maisha yako hupatikana pale unapopata ulichokuwa ukikitamani kwa muda mrefu. Lakini pia faraja hii huletwa na kuongezeka zaidi pale wewe mwenyewe kutoka moyoni mwako unapoamua kufurahi kwa kile kidogo au kikubwa ulichonacho.”alimalizi Ali Kiba. Na kwa mtazamo huu utaona ni jinsi gani kuna utofauti wa wasanii wengine wengi na msanii huyu wa kipekee mkongwe sana kwenye game la Bongo music.
Previous Post Next Post