Exclusive Audio: M-Rap kuwashirikisha marehemu Ngwair na Mwana FA kwenye remix ya Usiende Mbali

Rapper M-Rap Lion ambaye ni moja kati ya rappers wenye umri mdogo wanaofanya vizuri Tanzania, ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa atafanya remix ya wimbo wake ‘Usiende Mbali’ na kwenye wimbo huo atawashirikisha marehemu Ngwair na Mwana Fa.




Amesema kuwa ameamua kufanya remix ya wimbo huo kutokana na kushauriwa mara kwa mara na watu wake wa karibu kuifanyia kitu ngoma hiyo kwa kuwa ni kali na ni vyema iendelee kuwa na kitu kipya.

“Hapo mwanzo nilikuwa nafikiria niwaweke young rappers wenzangu au niwaweke ma-legendary hawa. Lakini at the end of the day nikawa nimepata solution kwamba ntafanya na two legends… wa kwanza ni the late Ngwair halafu wa pili ni Mwana Fa. Kwa hiyo hao ndio watu ambao nitafanya nao hiyo remix na itabadilika kidogo kwenye upande wa beat na itakuwa too live yaani.” M Rap ameiambia tovuti ya Times Fm.

“Juzi kati tu hivi studio alinipigia simu Maneck akaniambia kuna verse fulani ameisikia studio… kwa sababu Ngwair alikuwa akienda AM anarekodi tu anaweka verse nini. Maneck ndio akaniambia kuna verse fulani inafanana na nyimbo yako Usiende Mbali vilevile kwa hiyo kwa sababu aliipenda ile nyimbo ya Usiende Mbali akasema ‘mimi nitaitoa hii verse kama zawadi halafu itakuwa hii nyimbo kama remix halafu tutamtafuta mtu mwingine na itakuwa Usiende Mbali Remix’.”

Ameeleza kuwa chorus ya wimbo huo itabaki kama ilivyofanywa na Jux.

Msikilize hapa:



Source:Timesfm
Previous Post Next Post