Birdmen amzawadia Justin Bieber Bugatti

Muanzilishi na mmiliki wa studio ya Cash Money, mjasiriamali na rapa Brayan Williams(45) ‘BirdMan’ amemzawadia mwanamuziki wa R&B, Justin Bieber gari ya kifahari aina ya ‘Bugatti Veyron’ yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 2 alilokuwa akitumia hapo awali.

“Uncle Stunna luv. My first Bugatti ♛ #generosity,” aliandika Justin Bieber kwenye ukurasa wake wa Instagram sambamba na kuweka picha ya mkoko huo wa bei chafu.


Birdman na Justin Bieber





Bugatti aliloposti Justin Bieber Instagram baada ya kupewa kama zawadi na Birdman.



Kwa wale wafuatiliaji ni kwamba, gari alilopewa Justin Bieber ndio alilolitumia BirdMan kwenye video ya wimbo wake wa ‘Fire Flame’ iliyotoka mwaka 2010. unaweza ukautazama mkoko huo wa bei mbaya hapo chini.




Previous Post Next Post