Victoria Kimani : Asema anekutana na Diamond Platnumz mara moja tu, na wala sina namba yake ya simu


Hivi karibuni mwimbaji wa ‘Number One’ Diamond Platnumz alikanusha tetesi za huenda kuna kitu kilizaliwa baina yake na mwimbaji Mkenya Victoria Kimani baada ya kukutana hivi karibuni nchini Afrika Kusini.




Hisia hizo zilitokana na picha walizopiga pamoja wakiwa karibu walipoungana na wasanii wengine wakubwa wa Afrika kwaajili ya mradi wa ONE campaign.

Victoria ambaye makazi yake ni Nigeria naye ametoa yake ya moyoni kwa kukanusha juu ya tetesi hizo.

“Mimi sijui hizi tetesi zimetokea wapi”, Victoria aliiambia Nairobi News.




Alienedelea kusema,

“Nimekutana na Diamond mara moja tu, tulipokuwa tunarekodi wimbo wa ONE campaign huko Afrika Kusini wiki mbili zilizopita. Sina hata namba yake, so sijawasiliana naye toka tulivyokutana Afrika Kusini”. Alisema Kimani.


Chanzo: Nairobi Wire
Previous Post Next Post