Papa Francis atetea kanisa la Katoliki

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ametetea rekodi ya kanisa hilo katika utatuzi wa suala la unyanyasaji wa watoto unaofanywa na mapadri.


Katika mahojiano na gazeti moja la Italia, Papa Francis amesema kuwa hakuna aliyefanya zaidi kutatua swala hilo kuliko uongozi wa kanisa hilo.
Amesema kuwa kanisa hilo limewajibika katika kuchukua hatua za uwazi, lakini ndio taasisi inayoshambuliwa.
Mwezi uliopita Umoja wa Mataifa ulishtumu, utawala wa Vatican kwa kushindwa kukabiliana na suala la unyanyasaji wa watoto mbali na kuwaficha wanaotekeleza tendo hilo.

Chanzo:BBC
Previous Post Next Post