Wakazi adai Wanaijeria wengi wanadhani Diamond ni Mnaija, asema My Number 1 inahit kila kona

Rapper Wakazi aka The Bilingual Beast amesema wananchi wengi wa Nigeria wanadhani Diamond Platnumz ni msanii wa Nigeria.




Akiongea Wakazi ambaye alikuwa nchini Nigeria hivi karibuni ambako alikaa kwa takriban mwezi mzima alisema sababu ya Wanaijeria kuhisi Diamond ambaye jina lake halisi ni Nasib Abdul ni kutokana na makabila makubwa ya huko kutosikilizana.

“Kuna wengine wanafikiria Diamond ni underground wa Kinaijeria sababu Nigeria kuna makabila matatu makubwa ambayo hayasikilizani kwahiyo mtu akisikia wimbo asiouelewa atasema ‘itakuwa kabila fulani’,” amesema Wakazi.

Tazama video ya My Number 1 Remix ft Davido...!



Wakazi amesema wa Diamond My Number One aliomshirikisha Davido unahit nchini Nigeria na karibu redio, TV na club zote kubwa za huko zinaicheza. “Even in some radios ipo kwenye top 10, top 20 zao so a lot of people are aware of who Diamond is right now,” ameongeza.

“In general Diamond is doing good na ofcourse I am proud of him sababu ni mtanzania and the song is doing very well and they show it all the time and people dance to it even in clubs.”
Previous Post Next Post