Siri ya kuonesha 'mahaba mazito kwa mpenzi wake

Kwa wakaazi wa maeneo ya Pwani ya Afrika Mashariki wanafahamu maana halisi ya ‘mahaba ya njiwa’. Haya ni mahaba ambayo ni zaidi ya kikohozi na hayajifichi.
Kila uwaonapo njiwa utagundua wanagusana midomo mara kwa mara na kulindana-lindana. Hata kulalia mayai wanalalia wote wawili. Hayo ni mambo ya njiwa!



Hii ndiyo inamtokea mwimbaji wa Can’t Remember to Forget, Shakira na mpenzi wake mwana soka Gerard Pique ambao wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume, Milan mwenye umri wa mwaka mmoja.

Shakira ameelezea sababu zinazomfanya aoneshe kila alichonacho mpenzi huyo na kuonesha mahaba na ukaribu uliopitiliza.    Mwimbaji huyo ameiambia Us Weekly kuwa ni waaminifu kwa kila mmoja katika kila hali na kwamba kuwa ‘touchy touchy’ kwao inasaidia.

Aameongeza kuwa ilimchukua miaka mingi kutafuta mapenzi kwa hiyo hataki kumpoteza tena mpenzi wake huyo kwa chochote kile katika dunia hii.

“We are very honest, no matter what. And we are very touchy touchy. It works for us…it took me years tofind love, so I don’t want to lose him for anything in the world, that’s my priority.”

Shakira aliwahi kueleza kuwa Gerard Pique alimkataza kufanya video na wanaume wenye mvuto na alitii na kuamua kufanya video na wanawake. Na uamuzi huo ndio uliozaa video tata ya Can’t Remember to Forget You aliyofanya na Rihanna.
Previous Post Next Post