Master J Afunguka Wasanii wangu wanweza kurekodi sehemu yoyote hile. sio lazima kwa Marco Chali tu!

Unapoongelea Mj Records unaongela studio kuwa hapa Town na inayohit kwa namna ya kipekee Bongo, Kwa studio zingine zinazosimamia wasanii pia, ni ndoto kusikia wasanii wake wakifanya nyimbo kwenye studio zingine. Lakini hii ni tofauti kwa MJ Records.




“Record label sio studio, kazi yake ni kufinance, kumarket na kudistribute,” Master J alisema. “Mimi MJ Records wasanii wangu wana uwezo wa kurekodi sehemu yoyote kama mlivyoona sio lazima kwa Marco Chali tu. Na mimi ndio niliwaambia ‘jamani acheni tu kurekodi kwa Marco, lazima muwe na sound tofauti, otherwise mnakuwa mnawachosha tu mashabiki wetu’. Na unaporekodi studio tofauti hata sound unayopata inakuwa tofauti.”

Master J amesema kwa sasa wasanii walio chini ya MJ Records ni Shaa, Izzo B na Quick Rocka peke yake ambao aliwasainisha tena mkataba wa miaka minne kwa awamu ya pili. “Wale wengine ambao mikataba imeisha, sijarenew, wengi nimekataa sababu walikuwa hawana nidhamu.”
Previous Post Next Post