Kesi ya Chris Brown wanasheria wake wataka afutiwe kesi ya kushambulia

Wanasheria wa Chris Brown wamemtaka jaji kumfutia kesi iliyotokana na kumshambulia mtu hukoWashington.  Wanasheria hao waliazna kufuata taratibu za kisheria Jumatano wakidai kuwa muendesha mashitaka hakuitumia sheria ipasavyo katika kufungua kesi hiyo.

Hata hivyo muendesha mashitaka huyo bado hajajibu chochote wakati ambapo Chris Brown anaendelea kutumikia kifungo cha takribani mwezi mmoja jela.





October mwaka jana Chris Brown na bodyguard wake walikamatwa kufuatia tuhuma za kumshambulia mtu mmoja huko Washington, ambapo ilidaiwa kuwa wote walimpiga ngumi kadhaa mtu huyo.

Wakati mwimbaji huyo anakamatwa alikuwa chini ya kipindi cha matazamio alichopewa kufuatia kesi ya kumshambulia Rihanna mwaka 2009, na baada ya kukamatwa jaji aliamuru ahudhurie matibabu ya kudhibiti hasira.

Hata hivyo baada ya kuonekana amekiuka masharti ya Rehab, Chris alifukuzwa na kuangikia kwenye mikono ya jaji aliyemfunga jela.

Kesi yake itasikilizwa tena katikati ya mwezi April.
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa