Audio: Joh Makini kufanya ngoma mpya na Jaguar

Wiki hii members wa Weusi, Joh Makini, G Nako na Nikki wa Pili walikuwa Nairobi Kenya kwa ajili ya kutumbuiza kwenye uzinduzi wa video ya Navio wa Uganda.

Lakini kundi hilo liliitumia nafasi hiyo kujitangaza zaidi nchini humo pamoja na kufanya collabo ikiwemo Remix ya Gere na Rabit Sungura na mfalme wa rap Kenya Collo.




Joh aliiambia Bongo5 leo asubuhi kuwa wanatarajia kufanya wimbo na Nazizi muda wowote kwa kuwa Nazizi alikuwa amechoka wakati ambapo walipanga kufanya collabo.

Tovuti ya Times Fm imepiga story na Nikki wa Pili ambaye yuko safarini akirejea Dar es Salaam ambapo alidokeza kuwa amewaacha G-Nako na Joh Makini Nairobi wakimalizia mipango kadhaa na kwamba Joh Makini anatarajia kufanya wimbo na Jaguar.

“Jaguar na Joh mpaka beat imeshatengenezwa sema jamaa ana mambo yake mengi kwa hiyo hata kama kama wanataka kufanya pale lakini watakuja kuingizia sauti huku Tanzania lakini jamaa hana tatizo. Amesema Nikki wa Pili.

Ameeleza kuwa wawili hao wameshakubaliana kufanya kazi lakini muda ndio unaobana.




Previous Post Next Post