Drake na Rihanna ni wapenzi Rasmi

Wanasema penzi ni kikohozi… kama tunaamini huo msemo basi tunaweza kusema Rihanna amepaliwa na hawezi kuficha tena kuwa yeye na Drake ni zaidi ya marafiki bali wapenzi waliokolea.

Baada ya kuwepo tetesi nyingi kuwahusu, sasa imethibitishwa kuwa Drake na Rihanna ni wapenzi. Vyanzo mbalimbali vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Rihanna na Drake wametoka kwenye ukaribu wa kawaida hadi kuwa na uhusiano serious wa kimapenzi.


Mtandao huo umedai kuwa Rihanna anataka kutumia muda mwingi na Drake pindi muda wake ukimruhusu kwakuwa Drake anamtreat vizuri kuliko mwanaume yeyote aliyewahi kuwa naye. Wawili hao wamekuwa pamoja wakati ambapo Drake akiwa na ziara barani Ulaya na vyanzo vimesema kuwa wamekuwa pamoja kila siku tangu waonekana pamoja kwa mara ya kwanza.


Wiki hii, wawili hao walienda sehemu ambayo walitulia na kupata mvinyo, lakini baada ya muda Drake aliamka na kuelekea msalani.

Katika hali isiyo ya kawaida, Rihanna alionekana akimfuata Drake msalani na kuingia kwenye ‘choo’ cha wanaume hali iliyowafanya watu kupiga kelele na kuzungumza huku mtu mmoja akichukua video kwa simu ili kuutunza ushahidi.

Tazama video hapa chini..!

Previous Post Next Post