Chris Brown afungua kampuni yake ya modeling, ‘ Legendary Faces’

Super star anayehit kwa misukosuko tofauti Criss Brown, pamoja na kwamba weekend ya star huyu haikuwa nzuri kutokana na kulala lupango baada ya kufukuzwa rehab kwa mara nyingine, lakini biashara zake zinaendelea na sasa amewekeza katika biashara mpya ambayo ni tofauti na muziki.



Jumanne ya wiki iliyopita, mwimbaji huyo wa ‘Fine China’ kabla hajakutwa na maswahibu hayo alitangaza mradi wake mpya wa kampuni yake ya modeling iitwayo ‘Legendary Faces’ agency.


Breezy alitangaza kupitia tweeter huku akiweka link ya website mpya kwa kuandika ‘My Agency http://legendaryfacesmm.com casting by: @charlesincharge101 Photos by: @krishphotos @dgphoto7’.

Mshindi huyo wa grammy ambaye pia ameahidi kutoa album yake ya ‘X’ mwezi May mwaka huu baada ya kuahirisha mara kwa mara toka mwaka jana, alispend weekend yake lockup huko Los Angeles baada ya jaji kuamuru akamatwe kwa kuvunja sheria na taratibu za tiba yake, japo taarifa ya mahakama haikuelezea sababu halisi iliyomsababisha Brown aondolewe rehab huko Malibu alikokuwa ameongezewa miezi mingine miwili ya kuendelea kupata tiba ya kukabiliana na hasira.


Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa