Temba akabiziwa Nyumba na Said Fella

Said Fela amemkabidhi Mheshimiwa Temba nyumba yake ya pili. Rapper huyo wa TMK Family, amesema kuwa nyumba aliyokabidhiwa na Fela imepatikana kutokana na mauzo ya kazi zake za muziki ndani ya TMK Family.


Kupitia mitandao ya kijamii leo Said Fella Meneja na boss wa Tmk wanaume Family amemkabidhi nyumba Mheshimiwa Temba mjengo ambao uko Kimara Kilungule,na kumbukumbu Temba si msanii wa kwanza kukabidhiwa nyumba na Fella.

















Temba amesema kuwa utaratibu huo ulikuwepo toka zamani ambapo kila msanii kutokana na fedha alizoingiza kupitia kazi zake hununuliwa kiwanja au kujengewa nyumba.

Thamani yake bado hatujakaa kupiga mahesabu maana ujenzi wake ni wa kimaskini na ufahamu tukipata 100,000 elfu 20 kununua matofali elfu 80 kula na watoto,lakini tukikisikia inafika Milion 20 ina vyumba vitatu vya kulala,ina sehemu ya chakula,parking ya magari ziko mbili tumejenga mpaka sasa Temba na Chegge wana nyumba mbili mbili’.



Previous Post Next Post