Picha: Kikongwe akamatwa Chumbani kwa Mtu akiwa Mtupu, Inadaiwa ni Mchawi

Hili ni tukio lilitokea huko Bukoba ambalo linamhusisha Kikongwe mmoja ambaye jina lake bado halijapatikana kukutwa chumbani kwa mtu huku akiwa mtupu chumbani kwa mtu.Mpaka sasa bado haijajulikana kama ni Kigarura au pengine alipata matamani ya mwili akaona pengine chumba kile kingemfaa kumpatia msaada wa mambo yake.

 Kikongwe Aliyekamatwa akiwa mtupu chumbani kwa mtu..



Bibi Kizee huyo anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 70,ambapo amekamatwa alfajiri ya leo January 31 hata hivyo polisi wamefanikiwa kumnusuru na kifo baada ya kumchukua na kumpeleka kituo cha polisi.

Mashuhuda wa mwanzo wanadai walimkuta bibi huyo akitapatapa bila kujua nini la kufanya huku akiwa mtupu na nguo zake zikiwa pembeni kitendo kilichotafsiriwa kwamba pengine bibi huyo anaweza kuwa mchawi,huku wengine wakisubiri taarifa ya polisi na wengine wakisema huenda bibi huyo alipatwa na matamanio ya kimwili.





Chanzo: Bukobawadaublog.
Previous Post Next Post