Mmiliki wa Whatsapp itakayonunuliwa na Facebook kwa dola bil.19, aliwahi kutoswa ajira na Facebook na Twitter

Katikati ya mwaka 2009, Brian Acton alikuwa software engineer ambaye hakuna kampuni iliyotaka kumwajiri. Pamoja na uzoefu wa miaka zaidi ya 10 kama mwajiriwa wa Yahoo na Apple Computer, alitoswa kuajiriwa kwenye makampuni ya Facebook na Twitter.


Waanzilishi wa Whatsapp: Brian Acton na Jan Koum
Kwanza walikuwa Twitter waliomkataa mwezi May. Tarehe 23, May mwaka 2009, Brian Acton ‏alitweet: Got denied by Twitter HQ. That’s ok. Would have been a long commute.”
Kisha Facebook waliokataa kumchukua mwezi August. Tarehe 3 August, 2009 akatweet:Facebook turned me down. It was a great opportunity to connect with some fantastic people. Looking forward to life’s next adventure.”
Baada ya Acton kukosa kazi kwenye makampuni hayo, aliamua kuanzisha kitu chake mwenyewe. Aliamua kuungana na aliyekuwa mwajiriwa mwenzake wa Yahoo, Jan Koum, kuanzisha WhatsApp, ambayo leo imekuwa mfalme wa mawasialino ya ujumbe duniani. WhatsApp inatawala vichwa vya habari wiki hii sababu Facebook imekubali kuinunua kampuni hiyo kwa dola bilioni 19.

Akiwa na asilimia 20 ya hisa kwenye kampuni, Acton atakuwa tajiri wa dola bilioni 3. Historia yake imegeuka kuwa funzo la watu kutokata tamaa kwa wale wanaotafuta kazi. Story yake pia itawapa uchungu waajiri. Kuajiri watu sahihi ni jambo la bahati lakini hakuna kampuni kubwa duniani itapenda kuwa maarufu kwa kuacha Brian Acton mwingine aondoke.
Chanzo: Forbes
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA