Facebook Kuinunua Whatsapp kwa Dola Bilioni 19

Kampuni ya Facebook itainunua kampuni inayokuwa kwa kasi ulimwenguni ambayo inajishughulisha na huduma za utumaji wa ujumbe mfupi (mobile messaging), Whatsapp Inc kwa kiasi cha Dola Bilioni 19 pesa taslimu, ambapo pia watabuni njia za kuifanya iweze kufanya vizuri zaidi kwenye soko, ambapo walengwa wakuu ni rika la vijana.

Jan Koum, Mwenyekiti Mtendaji Na Muanzilishi, Whatsapp Inc,

Whatsapp imeweza kujizolea sifa kabambe ambapo ina watumiaji zaidi ya milioni 450, na taarifa zinaonyesha kuwa kila siku watumiaji wapya milioni 1 hujiunga na mtandao huu wa kijamii.

Teknolojia imekuwa ikipanuka kwa kasi, na malengo makuu ya mwenyekiti mtendaji wa Facebook, Mark Zuckerberg ni kupanua wigo huo, na kuwafanya watu waweze kufurahia huduma hizo kwa urahisi zaidi kupitia vifaa mbalimbali. (Smartphones, Ipads etc)

Hii si mara ya kwanza kwa Zuckerberg kufanya kitendo hichi, kwani tayari alinunua mtandao mwingine wa kijamii, maarufu kama Instagram ambao unatumia picha. Kwa kufanya hivyo, Facebook wanapigana vikumbo kwenye soko la dunia na mtandao wa kijamii wa Twitter na Snapchat


“Since WhatsApp and (Facebook) Messenger serve such different and important users, we will continue investing in both.”


Kupitia ununuzi huo, Mwenyekiti na muanzilishi wa Whatsapp, Jan Koum atajiunga kwenye bodi ya utendaji ya Facebook, ambapo Facebook watagharimia kiasi cha Dola Bilioni 3, ambazo ni juu ya zile dola bilioni 16 zitakazolipwa kwa manunuzi..

“WhatsApp will complement our existing chat and messaging services to provide new tools for our community,“aliandika Mwenyekiti mtendaji wa Facebook, Mark Zuckerberg.
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA