KTMA waelezea sababu za kukitoa kipengele cha mtayarishaji chipukizi, watayarishaji nao waongea

Waandaaji wa tuzo za KTMA, wameelezea sababu za kukiondoa kipengele cha Mtayarishaji wa muziki anayechipukia kwa madai kuwa wengi watakaoingia kwenye kipengele hicho mwaka huu ni wale wale waliotajwa mwaka jana.


Kilimanjaro Brand Manager, George Kavishe

Mratibu wa tuzo hizo kutoka Baraza la Sanaa Tanzania, BASATA, Kulwijira Maregesi alisema mpaka pale watakapojiridhisha kuongezeka kwa watayarishaji wenye vigezo hivyo ndipo kitakaporudishwa.

“Baada ya kupata maoni kutoka kwa wadau mbalimbali tukaona ni heri kwa mwaka huu tukiondoe mpaka pale tutakajiridhisha kuwa wameongozeka,” Maregesi alikiambia kipindi cha Showtime Next Chapter cha RFA jana. Maregesi alisema sababu ya pili ni kuwa wengi wa watayarishaji hao hawatambuliki na BASATA.

Kwa upande wake mtayarishaji wa wimbo wa Snura, Majanga aitwaye Mo Fire, alisema kuondolewa kwa kipengele hicho kumemvunja moyo.

“Imenishusha tembo kwa kiasi fulani hivi, nimejisikia vibaya kwakweli, nimeona kwanini sasa wametoa hizi issue,” amesema Mo Fire. Aliongeza kuwa kwakuwa kimebaki kipengele cha mtayarishaji bora peke yake, kwa wale walioanza kama yeye kutajwa kuwania tuzo hiyo ni ndoto.

Naye producer wa De Fatality, Mesen Selekta ambaye mwaka jana alishinda kipengele hicho, anasema kuondolewa kwa kipengele hicho kutapunguza motisha kwa watayarishaji wachanga. Amesema baada ya kupata tuzo hiyo, alipata moyo zaidi wa kufanya kazi nzuri ili kutimiza ndoto zake.

Previous Post Next Post