Picha: Clouds FM yaukaribisha mwaka 2014 kwa Kushiriki Katika Kutoa Misaada, Ni Katika Kusheherekea Miaka 14 ya Kuzaliwa Kwake

Kituo cha Redio namba moja hapa nchini, Clouds FM jana kimefikia kilele cha mwezi wa maadhimisho ya miaka 14 toka kimeanzishwa. Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika kwa mwezi mzima sasa, yalianza na watangazaji wa vipindi tofauti kwenda mikoa mbalimbali ili kuweza kusherekea miaka hii 14 pamoja na wasikilizaji wao sehemu walipo.

Baadhi ya wafanyakazi wa Clouds FM wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake waliokuwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Temeke, baada ya kukabidhi misaada yao ikiwa ni sehemu
Msanii wa mashairi na kughani, Mrisho Mpoto akikabidhi msaada wa pedi za watoto kwa Mama Leah Othman katika hospitali ya Temeke ikiwa ni katika kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM
Mtangazaji wa Jahazi, Ephraim Kibonde akimfariji mmoja wa akina mama katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Temeke

Mtangazaji wa kipindi cha Ampilifaya, Millard Ayo akimhoji mmoja wa vijana ambao wameacha kutumia madawa kwa msaada wa kituo cha Keko Youth

“Maadhimisho haya ya miaka 14 kwa mwaka huu yana lengo moja kubwa, kuwashukuru wasikilizaji wetu kwa kutufikisha hapa tulipo, na ndio maana tumeanza kwa kuwapa misaada wanaohitaji, halafu tunamalizia kwa burudani,” alisema Kusaga. Akielezea zaidi mafanikio ya Clouds FM kwa kipindi cha miaka 14, Kusaga alisema redio imefanikiwa kuwafikia watu wengi zaidi, imeongeza ubunifu lakini pia kumekuwa na uboreshaji wa hali ya juu wa mitambo ya kutangazia pamoja na maudhui.

“Kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo tumefanikiwa kushinda tuzo ya Super Brand, na kwa mwaka huu pekee radio imefanikiwa kuanza kusikika mikoa ya Njombe, Songea, Njombe, Sumbawanga, Katavi na Geita, kupitia mitandao kwa wasikilizaji wetu nje ya nchi lakini pia tumefanikiwa kufanya tamasha la Fiesta kwa mafanikio zaidi.”


Mtangazaji wa kipindi cha Ampilifaya, Millard Ayo akiwa amempakata mtoto, baada ya kutembelea hospitali ya Temeke na kukabidhi misaada ikiwa ni sehemu ya miaka 14 ya Clouds FM

Jana ikiwa ndio siku ya kilele cha maadhimisho hayo, Clouds FM imetembelea hospitali ya Temeke na kituo cha kuhudumia vijana wanaotumia madawa ya kulevya cha Keko Youth, ambapo misaada mbalimbali imetolewa.

Wakiwa katika hospital ya Temeke, Clouds FM imetoa vifaa mbalimbali vya hospitali katika wodi ya wanawake na watoto, huku Keko Youth wakipewa vitendea kazi ambavyo vitawezesha vijana kujiajiri baada ya kumaliza matibabu.
Akizungumzia maadhimisho hayo ya Clouds FM, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga alisema sherehe hizi kwa mwaka huu ni za kipekee kwa Clouds FM hasa kwa kuwa wameweza kufanikisha mambo mengi makubwa toka walipoanza.

Wafanyakazi wa Clouds FM wakikabidhi vifaa kwa wawakilishi wa hospitali ya Temeke ikiwa ni katika kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM


Mtangazaji wa Kipindi cha Power Breakfast, Paul James (PJ), akikabidhi msaada wa pedi kwa mmoja wa wakina mama walio katika wodi ya wazazi wa hospitali ya Temeke

Kusaga pia aligusia mchango wa Clouds FM katika kuhamasisha maendeleo na uzalendo hapa nchini akitoa mfano wa semina za Fursa ambazo zilifanikiwa kwenda nchi nzima zikizungumza na vijana kuamka na kuchangamkia fursa katika sehemu wanazoishi.

“Semina za Fursa zimekuwa mfano mkubwa namna Clouds FM ilivoweza kutumia nguvu yake kama radio inayosikilizwa zaidi katika kuchagiza maendeleo, na kwa hakika mafanikio ya semina yamekuwa ni makubwa sana,” alisisitiza Kusaga.

Kusaga pia alitoa shukrani za pekee kwa watanzania kwa kuinga mkono Clouds FM sio kwa kusikiliza tu bali hata katika kuhudhuria matamasha na shughuli nyingize za Clouds.

Wafanyakazi wa Clouds FM wakikabidhi vifaa kwa wawakilishi wa hospitali ya Temeke ikiwa ni katika kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM


Source:Bongo5
Previous Post Next Post