Mama Kanumba aandaa tamasha la kumsaka kijana atakayefanana na Steven Kanumba

Mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema anaandaa tamasha maalum la kumsaka kijana atakayeigiza kama Kanumba katika filamu yake baada kukosa star katika kiwanda hicho anayeweza kucheza nafasi hiyo.


Akizungumza na Centre Spread ya Global Publisher,Mama Kanumba alisema mastaa wengi wa filamu wanatamani awape nafasi ya kucheza kama Kanumba katika filamu yake anayoiandaa ambayo inayohusu maisha ya mwanaye tangu utotoni, na kudai katika wote hajaona mwenye kigezo cha kumpa nafasi hiyo.

“Sio kwamba hawana kiwango kizuri cha kumfikia mwanangu, isipokuwa kwa mtazamo wangu naona nikimshirikisha staa yoyote katika kipengele hicho nitakuwa nimevurunda kazi yangu…nitaandaa tamasha maalumu la kumsaka kijana anayefanana na Kanumba,”alisema.

Previous Post Next Post

Popular Items