Michael Essien kwenda AC Milan

Kutoka darajani Stamford Bridge, klabu ya Chelsea imethibitisha kufikia makubaliano na klabu ya Italia, Ac Millan juu ya uhamisho wa kiungo mkabaji, Michael Essien ambaye sasa anajiunga na klabu hiyo baada ya vipimo na makubaliano kuridhiwa.



Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ghana, ambaye msimu uliopita alichezea kwa mkopo klabu ya Hispania, Real Madrid ambapo alikuwa akijitahidi kufanya vizuri kwenye mechi kadhaa. Tangu msimu wa ligi kuu ya uingereza uanze wa 2012-13, kiungo huyu mwenye umri wa miaka 31, mara baada ya kurejea kutoka Real Madrid, amefanikiwa kuanzishwa mara mbili tu kwenye kikosi hicho cha “The Blues”.

Essien aliekea Milan Ijumaa jioni na kupokelewa vyema na mashabiki wa timu hiyo wakiwa na t-shirt zenye jina lake kuonyesha furaha yao kwa yeye kuwasili klabuni hapo.

“I’m happy being here”, alisema Essien alipohojiwa na chaneli ya Ac Milan. Aliongeza kwa kusema, “I will do my best for Milan and i hope to be ready to play”
Previous Post Next Post