STORI ULIZOMISS KUTOKA KATIKA MAGAZETI YA UDAKU: BOB JUNIOR ATESWA NA KUACHWA

Magazeti ya udaku yameendelea kumwandama Mtaarishaji wa Muziki na Mwanamuziki Bob Junior kiasi ambacho ameamua kusema ‘inatosha sasa’.


Bob Junior, mke wake na mtoto wao

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii anayoitumia staa huyo, Bob Junior ameyalaani magazeti hayo kwa kuendelea kuikuza habari ya kuachana na mkewe wake kutokana na kile yalichodai kuwa (mkewe) alikuta nguo ya ndani ya mwanamke mwingine.



“Ahsanteni sanaa hii imekuwa too much sasa kila nikiomba muache hamtaki hamna story nyenginee jamanii,”ameandika Bob Junior kwenye picha ya gazeti la udaku lililoandika habari yenye kichwa cha habari kisemacho: Kufuli ya kike aliyofumaniwa nayo Bob Junior ni yake’.

Juzi pia alilalamika baada ya gazeti la udaku kuandika habari yenye kichwa cha habari: Ndoa ya Bob Junior Chali.

“Leo tena jamani hakuna habari nyingine hata kama nimeachana naye kanizalia napaswa kuwekewa heshima mwanangu akija kuwa mkubwaa nita mwambia nini mimi inaniumaa Bob Junior tuu akilala akiamkaa ni Bob junior kila sehemu.”

Habari ya kwanza kuandikwa na gazeti hilo la Sani kuhusiana na kisa hicho ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho: Sidiria, Chup* yavunja ndoa ya Bob Junior.

Previous Post Next Post