DIRECTOR MKONGWE WA TASNIA YA BONGO MOVIE WILLIAM MTITU APATA MTOTO WA KIKE

Mwigizaji, muongozaji wa filamu na mmiliki wa kampuni wa filamu ya 5effects William Mtitu amepata bahati ya kuongeza idadi ya wanafamilia wake baada ya mke wake Jovitha Mtitu kujifungua salama mtoto wao wa kwanza kwenye hospitali ya Regency jijini Dar es salaam hivi majuzi.





Kupitia ukurasa wa mtandao mmoja wa kijamii Mtitu aliandika…

“Nawashukuru madaktari wa hospital ya regency na kwa Dr mvungi wakiongozwa na Dr getu kwa kusaidia mpaka mke wangu kujifungua salama na sasa naitwa baba na mke wangu mama ,kwa kweli mungu awabaliki sana…”

Hali ya Mama na mtoto ni njema na wanaendelea vizuri. Hongera sana Mtitu na familia yako.

Previous Post Next Post

Popular Items