BABAY MADAHA ANAKUJA NA FILAMU YAKE INAYOITWA "THE GAL BLADDER" CHINI YA KAMPUNI ILIYOMPA GARI YA CANDY N CANDY

Mwanamuziki na Actor wa Filamu Bongo Baby Madaha kutoka Tanzania ambaye kwasasa yuko chini ya label ya Candy n Candy ya Kenya, baada ya kutoa video yake mpya sasa anatarajiwa kuja na filamu mpya ya Kiswahili ‘The Gal Bladder’.


Kwa mujibu wa mtandao wa GHAFLA wa Kenya, filamu hiyo inaweza kuachiwa hivi karibuni. Baby Madaha amekuwa katika headlines mfululizo kwa siku za karibuni kutokana na mambo mengi anayoyafanya, kitu kinachoashiria matunda ya mkataba wake na Candy n Candy.


Hivi karibuni msanii huyo amezindua begi ndogo za kubebea zawadi ‘gift bags’ zenye picha yake, na aliiambia tovuti ya TIMES FM kuwa mradi wake utakaofuata ana mpango wa kuja na vifaa vya watoto kama toys.
Previous Post Next Post