AUDIO: MR BLUE AZUNGUMZA NA RADIO CITIZEN KUHUSIANA NA UTAPELI UNAOFANYWA KUPITIA JINA LAKE UKO KENYA

Hitmaker wa Mapozi, Mr Blue leo amezungumza na mtangazaji wa Radio Citizen, Willy M Tuva kwenye kipindi cha Mambo Mseto kuhusiana na jinsi ambavyo jina lake limeendelea kutumika kufanya utapeli nchini Kenya. Gazeti la The Star la Kenya liliandika kuwa staa huyo alitapeli advance ya show mbili za Kenya na kumfanya promota wa show hizo afungue kesi mjini Mombasa na kumuita Mr Blue ni tapeli na kwamba anatafutwa na polisi.

Mr Blue amesema promota huyo aliwasiliana na Mr Blue fake na wakakubaliana kuhusu show hizo lakini baadaye akawa ameingia mitini.

“Mwisho wa siku kumbe sio mimi. Jamaa amekuja kunipigia simu ananilalamikia nikamwambia ‘mimi sijui chochote, kwanza sipo kwenye Facebook’”, amesema Kabayser. Amesema hakuwa na kitu cha kumsaidia promota huyo kwakuwa alikuwa tayari na show zingine hapa nchini na hivyo asingeweza kuokoa jahazi.

“Jamaa akawa ameendelea na show zake, watu wakafanya fujo huko, at the end of the day nakuta ameandika kwenye magazeti kwamba ananitafuta na polisi. Mimi nikawa nimenyamaza tu sababu jamaa sijamkosea chochote, sio mimi niliyeongea naye, amedanganywa na watu,” amesema Blue na kuongea kuwa hajawahi kupewa hela na akashindwa kutokea kwenye show.

Blue amesema tayari mtu huyo amemfungulia mashtaka kwakuwa ameendelea kutapeli watu wengi hata nchi za nje. Alisisitiza kuwa kwa muda mrefu hayupo kabisa kwenye mtandao wa Facebook wala Twitter na kwamba mtandao anaoutumia ni Instagram peke yake.

Katika hatua nyingine, Mr Blue amekanusha pia taarifa kuwa alifanya mahojiano na kituo cha radio cha QFM kuwa amemshutumu msanii wa Kenya, Willy Paul, muimbaji wa gospel kwa kutumia Bongo Flava kuwa mwizi wa nyimbo. Kwenye mahojiano hayo Mr Blue fake ambaye ana lafudhi ya watu wa Mombasa alisema Willy Paul ameiba wimbo wa Belle 9 ‘Masogange’ na kurekodi wimbo wake ‘Mapenzi’.








“Mimi sikufanyiwa mahojiano nikamzungumzia Willy Paul wala sina muda wa kumzungumzia Willy Paul, sijui Willy Paul whatever you call him sababu simjui wala sijui anafanya muziki wa aina gani, nawezaje kumzungumzia?”

Willy Paul


Previous Post Next Post