MR BLUE AKANA KUHUSIKA KATIKA UTAPELI KENYA, ADAI KUNA MR BLUE "FAKE"

Hitmaker wa ‘Pesa’ Mr. Blue aka Kabayser amesema si yeye anayetafutwa na polisi huko Kenya kutokana na kudaiwa kulipwa hela ya show ya mjini Mombasa na kushindwa kuhudhuria. Amesema yupo mtu anayetumia jina la Mr. Blue kuwatapeli watu.



Kabayser amesema anashangazwa kwa kuzagaa taarifa kwamba anatafutwa na polisi nchini Kenya kwasababu ya utapeli.

“Sikuwa na show Kenya wala nini,ni waongo tu, kuna jamaa aliniambia kuna mtu amemlipa hela kwaajili ya kufanya show Kenya,ambaye anajiita Mr Blue halafu hajatokea. Mimi nimewaambia wametapeliwa na watu wa kwenye mitandao ,kama wana uhakika ni mimi waje nyumbani wanikamate,” amesema Blue.

“Unajua huwezi fanya show nje ya nchi kama Kenya bila kuwa na mkataba,kama wao wana mkataba na mimi nimechukuwa kiasi cha pesa kwajili ya show waanike hadharani watu waone.”

Aliongeza kuwa kama kweli walikuwa na nia na yeye akafanye show huko Kenya hawakutakiwa kufanya mawasiliano kwa njia ya Facebook bali wangetumia mawasiliano ya uhakika.

Gazeti la The Star la Kenya limeandika habari yenye kichwa cha habari: ‘Bongo sensation Mr Blue wanted by Kenyan authorities’ inayosema:

TANZANIAN bongo musician Kherry Sameer Rajab popularly known as Mr Blue is being sought by Kenyan police.

The Mapozi hit-marker is wanted for allegedly failing to show up for contracted performances at various entertainment joints in Mombasa. The singer failed to turn up at the Office Restaurant, Likoni and Mariakani Jubilant Hotel, on November 16 and 17 respectively.

According to event organiser Sammy Ondwar Onyango, he took the matter to the police because he had already paid the singer part of the agreed performance fee.

“Mr Blue is a very dishonest man. He even let me down during 2012 show at Jet Bar, Likoni, after he alleged that he had missed the bus to Mombasa and I was forced to to dig deeper into my pocket to book him on another bus. In the latest incident, we had agreed to pay him a total sum of Sh100,000 and I had already sent him Sh40,000 through M-Pesa. The matter is being handled by Likoni Police Station,” he told Word Is.

We contacted Mr Blue over the phone to respond to the claims, but the singer only replied via a short text message that he was driving and would call back later. His phone has since been turned off.
Previous Post Next Post