Picha: Rihanna auvaa utamaduni wa Abu Dhabi

Robyn ‘Rihanna’ Fenty anamashabiki kila kona ya dunia, ndio sababu baada ya kuandika historia Afrika Kusini weekend iliyopita aliipeleka ziara yake ya ‘Diamonds World Tour’ katika Falme za Kiarabu (UAE).

Ili kuhakikisha anawashika vilivyo mashabiki wa Abu dhabi, RiRi aliamua kuvaa mavazi yanayoendana na utamaduni wa mwanamke wa nchi hiyo ya Kiarabu unaomtaka kuvaa mavazi yanayofunika vizuri mwili wote na kuacha sehemu ya uso peke yake kwa sababu za kidini.

Riri (25) aliamua kushare na mashabiki wake wa dunia kwa kuweka pozi na kupiga picha mbele ya msikiti uliko Abu Dhabi na kuzipost Instagram.

Kwa Rihanna haikuwa tu kukidhi matakwa ya sheria ya mavazi ya nchi hiyo bali alihakikisha anaitumia fursa hiyo kama ukurasa mwingine wa fashion.


Baada ya Abu Dhabi Rihanna anatarajiwa kutua Tel Aviv, Israel kwaajili ya muendelezo wa tour yake, ambapo ataperform Leo Jumanne 
Previous Post Next Post