KKweli Hii ni Kali....Mtoto wa miaka miwili ajifungua ‘mtoto’


Mtoto wa miaka miwili wa Huaxi nchini China, amefanyiwa upasuaji wa kujifungua baada ya madaktari kugundua kuwa alikuwa na mimba.
article-2439498-1869504E00000578-235_634x416
Xiao Feng, alipelekwa hospitali baada ya tumbo lake kuwa kubwa kiasi ambacho alijikuta akishindwa kupumua.
Alipolazwa, madaktari walichukua picha za x-rays na MRI ba kugundua kuwa Feng alikuwa amebeba mimba isiyokua na hivyo kuamua kumfanyia upasuaji.
article-2439498-1869505900000578-951_634x418
Waliiondoa mimba hiyo changa iliyokuwa na upana wa cm 20 na tayari ilikuwa imeanza kuwa na vidole. Mimba hiyo ilitakiwa kuwa pacha wa mtoto huyo (yaani mmoja alikulia tumboni mwa mwenzie). Pacha huyo wa sponji angekua na kuwa mtoto wa kiume.
article-2439498-1869A2B000000578-917_634x431
Feng akiwa amebebwa na mama yake baada ya upasuaji
Mapacha wanaofanana hutokea pale yai linapojigawa wakati wa urutubishaji na mapacha walioungana hutokea pale yai linaposhindwa kujigawa.
Previous Post Next Post

Popular Items