Megan Lynne Young, aliyezaliwa tarehe 27 February 1990 ndiye Miss World 2013 aliyeshinda kwenye fainali zilizofanyika weekend hii kisiwani Bali, Indonesia.
Alizaliwa Marekani ambapo mama yake ni Mfilipino na baba yake ni Mmarekani. Akiwa na miaka 10 alihamia kwenye jiji la Olongapo nchini Ufilipino na kuendelea na masomo huko. Kwa sasa anasomea Digital Film Making.
Alianza kuwa maarufu baada ya kuwa housemate kwenye shindano la Pinoy Big Brother: Celebrity Edition 2 na kupewa jina “The Princess of Charm”. Ameigiza filamu kibao zikiwemo The Reunion na mwaka huu ameonekana kwenye tamthilia za Never Say Goodbye na Misibis Bay.
Pamoja na kuigiza, Megan amekuwa mtangazaji wa TV kwenye vipindi mbalimbali.
Megan Young ndio Mfilipino wa kwanza kuwahi kutwaa taji la Miss World tangu lianze mwaka 1951.
Tags:
Miss World