Jennifer Lopez adaiwa Kuachana na ‘Serengeti Boy’ wake Casper Smart


Jennifer Lopez na dogodogo wake Casper Smart wanadaiwa kuwa wamemwagana baada ya kudumu kimapenzi kwa kipindi cha miaka miwili



J.LO mwenye miaka 44 anadaiwa kulikatisha penzi na dancer wake huyo wa zamani mwenye miaka 26, na kumfukuza nyumbani kwake. Hata hivyo kuna vyanzo vingine vimedai kuwa wapenzi hao hawajaachana bado ingawa dalili za kuachana siku za usoni zipo.



Sababu kubwa ambayo wawili hao wamekaa muda huo ni kwasababu watoto mapacha wa Jennifer, Max na Emme wana uhusiano wa karibu na Casper, kwa mujibu wa EOnline


Source:EOnline 
Previous Post Next Post