Jaguar amsaidia Seneta wa Nairobi Mike Sonko kuwashawishi vijana wa Dondora kusalimisha silaha zao za moto

Jaguar anaweza kukatiza mitaa ya Dondora jijini Nairobi usiku wa manane na tena akiwa kwa mguu na wahuni wasimpige kabali aka ngeta. Wanamfahamu sana na kwao ni mwana tu.
Mike Soko (kulia) akikabidhi cheki kwa kijana anayewakilisha kundi lililosamilisha silaha. Katikati ni Jaguar

Hii ni kwasababu, hivi karibu hitmaker huyo wa Kigeugeu alifanikisha kitu kikubwa kwa kumsaidia Seneta wa jiji la Nairobi, Kenya, Bitoz Mike Sonko kuwashawishi vijana wa Dondora kusamilisha silaha zao za moto.

Wiki iliyopita, kulikuwa na story kuwa vijana waliokuwa na silaha kutoka Dandora na Korogocho jijini humo waliingia kwenye vita kali na kutupiana silaha kutokana na kugombania eneo la kutupia takataka. Polisi waliingilia kati kuepusha shari lakini hatua zaidi zikabidi zichukuliwe.

Jaguar akibadilisha mawili matatu na afisa wa polisi

Inasemekana kuwa mmoja wa vijana waliohusika kwenye vita hiyo alimpigia simu Jaguar ili aje kuwa kama msuluhishi kati yake na Seneta wa Nairobi, Mike Sonko ili wajadili uwezekano wa vijana hao kusamilisha silaha zao bila kukamatwa.

Mkutano huo ulipangwa na Jaguar na Sonko walikutana na moja makundi hayo maeneo ya Buru Buru na ambao wakakubali kusalimisha mitutu yao.
Mike Sonko na Jaguar pamoja maofisa wa polisi kwenye mkutano na vijana hao

Katika mkutano huo pia, maafisa wa juu wa Polisi walihudhuria.
Mike Sonko akiwa ameshika silaha iliyosalimishwa na vijana hao

Baadaye, Jaguar na Sonko walikutana na kundi jingine ambalo liliahidi kudumisha amani. Kundi hilo lilipewa pia cheki ya shilingi 100,000 za Kenya ili ziwasaidie kuanzisha biashara.

Jaguar na vijana hao wakiwa kwenye mkutano kwenye ofisi ya Seneta wa Nairobi

Source: Ghetto Radio 
Previous Post Next Post