Diamond Aongelea Kuvuja kwa Wimbo wake wa "KAMA NIKIFA KESHO"



Wakati wimbo wa My Number One’ wa Diamond ukiwa unaendelea kufanya vizuri katika chati mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, wiki hii kuna wimbo wake mwingine unaitwa ‘Nikifa Kesho’ umevuja na kusambaa kimya kimya kwenye mitandao.



Sio mara ya kwanza kwa nyimbo za Diamond kuvuja lakini sababu ya kuvuja kwa wimbo huu wa sasa ‘Nikifa Kesho’ iliyotolewa na Platnumz ni hii,
“Kuvujisha Nyimbo yangu hakuwezi kunipunguzia wala Kunidhuru chochote… Sanasana utanizidishia Umaarufu na kunipa Show zaidi… Kama nimeacha kurecord nyimbo Studio kwako Uspanick, Relax.. tafta Msanii mwingine Mkali zaidi yangu umrecordie Ngoma Ahit kushinda mimi….ila Kuvujisha Unajisumbua bure!”. ameandika ujumbe huo muda mfupi uliopita Kupitia instagram.
Pamoja kuwa hajatajwa kwa jina, lakini producer ambaye amekua akifanya naye kazi kwa muda mrefu kipindi kilichopita ni Manecky wa A.M Records, na hit song yake ya sasa ‘Number One’ ameifanya kwa Sheddy Clever, hivyo ‘kuna uwezekano mkubwa’ producer anayezungumziwa katika ujumbe huo akawa ni Manecky!!
Previous Post Next Post