Diamond Afunguka: Akanusha Kurudiana na Wema Sepetu



Baada ya minong’ono mingi iliyosambaa kwenye magazeti ya udaku kuwa Diamond na Wema Sepetu wamerudiana tena, hitmaker huyo wa Number One, ameamua kufunguka na kuusema ukweli.



Kupitia Facebook, NA blog yake Diamond amesema habari hizo si za kweli na kwamba yeye na Penny bado wapo pamoja na mapenzi yapo motomoto

Aliandika hivi...."  Kumekuwa na Uvumi na Habari nyingi sana 
Mitandaoni na Kwenye Media tofauti... kwamba mimi na Mwanadada
Wema Sepetu tuna mahusiano ya Kimapenzi, kitu
ambacho Sikweli na taarifa hizo ni za uongo.. uvumi huu ulianza kisa tu 
yeye kucomment kwenye Account yangu ya Instagram?..



Hebu tujifunze kubadilika, inamaana watu mkiwa hamko
kimahusiano ya Mapenzi basi msizungumze ama Kushiriki kwa chochote? 
Futeni huo uzamani na Mbadilike, inamaana 
Mnapenda kuona watu wanauadui... nimuda
wa kufanya kazi ili Kulipa sifa na heshima Taifa la Tanzania
na si kuekeana chuki zisizo nanfaida..
I REAL LOVE MY PENNY,SIJARUDIANA NA WEMA.  "
Previous Post Next Post

Popular Items