BABAY MAKING SWAG YA GOSBY KUPATIKANA KWENYE MIXTAPE YA COST2COST



Unapoongelea wakali wa kufanya mixtape Bongo, uwezi kumkosa Gosby katika list ya wale wasanii wanaofanya gemu ya Bongo kama mbele..na kama utakuwa ufahamu Gosby anafanya nini au ni nani. sikiliza Ngoma hiyo iliyoingia kwenye mixtape hii hapa chini hapa chini



Gosby ni msanii kutoka Tanzania anayefanya kazi tofautitofauti ni msanii anayejua kufflow kwa swag za kipekee. 
Gosby Anangoma mpya ambayo imepata shavu la kuingia  kwenye(mixtape) namba 1 duniani, ya Coast2Coast Vol 251 ya nchini Marekani.


picha hapo chini inaonyesha profile ya Gosby katika website ya COAST 2 COAST MIXTAPE VOL 251 Ambayo iko Hosted by Plies

fff
Hadi sasa, BMS inashika nafasi ya 9 kati ya nyimbo 40 zilizoingizwa kwenye kinyang’anyiro hicho ambapo nyimbo 20 tu ndizo zitakazopata fursa ya kuingia kwenye mixtape hiyo. Fursa hiii tampaGosby nafasi ya wimbo wake wa BMS kusambazwa kwa wadau na wapenzi wa muziki zaidi ya 2,000,000 duniani.
Kwa kushika nafasi ya 9 ni kwamba Gosby tayari ameshaingia kwenyemixtape ya coast2coast lakini kura zaidi zinahitajika ili aweze kuendelea kukaakileleni au hata kufika nambari moja. Mwisho wa kupiga kura ni October 8.
Coast2coast ni nini?
Coast2Coast ni kampuni ya kimarekani inayojishughulisha na usambazaji na promosheni za mixtapes duniani.
Coast2Coast mixtapes ni mixtape zinazokuwa downloaded kwa wingi zaidi duniani na zimepata zaidi ya downloads Million 200 tangu zilipoanzishwa miaka kadhaa iliyopita.
Miongoni mwawasanii ambao wameshawahi kufanya kazi na coast2coast mixtapes ni pamojana 50 cent, Snoop Dogg, Wiz Khalifa, Big Sean, Game, Pharrell, Nas, Lupe Fiasco, Chris Brown, LL Cool J, Fabolous, Gym Class Heroes, Flo Rida na wengine wengi. Vile vile madj kama Dj Drama, DjKhaled, Bigga Rankin, Dj Ill Will na wengine wengi.
Kila toleo la mixtape za Coast2Coast husambazwa kwa watu zaidi ya million 2 duniani na hupostiwa kwenye zaidi ya websites/blogs 1000 maarufu za muziki duniani ambazo kwa ujumla hupata downloads zaidi ya 500,000 kila toleo. Vilevile kila toleo husambazwa na wasambazaji zaidi ya 400 ambao husambaza copies katika majimbo kadhaa nchini Marekani, Africa na Ulaya.
JINSI YA KUPIGA KURA
Ingia kwenye link hii Ili uipigie kura ngoma kali ya gosby.. http://coast2coastmixtapes.com/audiodetail.aspx?audioid=270668
Upande wa mkono wako wa kulia utaona neno VOTE by FACEBOOK or TWITTER kama uko facebook basi piga kura yako kwa FACEBOOK na kama uko TWITTER piga kura yako kwa TWITTER.
Previous Post Next Post