WestGate Mall: Mpwa wa Rais Uhuru Kenyatta amabaye ni Marehemu kwa sasa alipigwa risasi 8 baada ya kumkinga mchumba wake aliyeuawa pia


Mtoto wa binamu yake na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Mbugua Mwangi ambaye ni miongoni mwa watu waliouawa na magaidi kwenye shambulio la mall ya Westgate jijini Nairobi, anadaiwa alipigwa risasi 8 baada ya kumkinga mchumba wake Rosemary Wahito dhidi ya magaidi hao.
0007e673-642
Mbugua na Rosemary walienda Westgate kununua pete za ndoa tayari kwa maandalizi ya harusi yao
Taarifa zinadai kuwa Mbugua na mchumba wake walikuwa wameenda kwenye mall hiyo kufanya shopping ya pete za ndoa, siku chache tu baada ya kuzitaarifu familia zao kuhusu mipango yao ya ndoa. Kwa mujibu taarifa hiyo, Mbugua alikuwa tayari ameshatoka nje baada ya magaidi hao kuishambulia mall hiyo na alipogundua kuwa mchumba wake alikuwa bado ndani alirudi kumuokoa na kukutana na na mauti hayo.
4_Mbugua_Mwangi
Mbugua aliuawa katika harakati za kumlinda mchumba wake
Kwa mujibu wa mashuhuda, wapenzi hao walikuwa pamoja pindi magaidi hao waliokuwa na silaha kali walipowaona, na Mbugua alimkingia kifua mchumba wake na hivyo kupigwa risasi 8 za moto. Wote waliuawa.
Mbugua alikuwa mtoto wa Catherine Mwangi (balozi wa zamani wa Kenya nchini Ireland) ambaye ni dada wa seneta Beth Mugo na mwanasiasa wa zamani Ngengi Muigai ambao ni mabinamu wa Rais Uhuru Kenyatta.
Hii tunaiita True Love….
Source: Niaje.com
Previous Post Next Post

Popular Items