Baada ya kufanyiwa marekebisho na kuwekewa vifaa vipya na vya kisasa, studio ya Kiri Records sasa itakuwa chini ya producer mwingine aitwaye Rash Don.

Akiongea na Bongo5, Kiri ambaye ndo mmiliki wa Kiri Records amesema hadi sasa producer huyo ameshafanya kazi na wasanii mbalimbali wakiwemo Ney Lee, Dullayo, AT na Ally Nipishe.

Kiri amesema studio hiyo imeongezewa vipya ambapo kwa sasa inapatikana maeneo ya Kinondoni Studio, barabara iendayo Sterio opposite na FJ Hotel zamani Livingstone.

Awali producer wa studio hiyo alikuwa ni C9 ambaye kwa sasa amefungua studio yake mwenyewe.