Picha: Kim Kardashian akiwa na toleo jipya la iPhone 5s kabla ya tarehe rasmi ya kuanza kupatikana kwa simu hizo



Mama wa North na ubavu wa rapper Kanye, Kim Kardashian ameamua kuwajulisha mashabiki wake kuwa yeye anaenda zaidi ya wakati na wakati kwa kuwaonesha kuwa mtoto mpya wa ‘Apple’ anayesubiriwa kwa hamu iPhone 5S tayari yuko kwenye mikono yake kabla hata ya tarehe rasmi ya kuanza kupatikana kwa wateja wote.


Kupitia Instagram Kim Kardashian amepost picha akiwa na simu hiyo

Kwa mujibu wa mtandao wa Apple iPhone 5S zitakuwa zikipatikana katika rangi tatu gold, silver na gray na zitaanza kupatikana Marekani, Australia, Canada, China< Ufaransa, Ujerumani, Hong Kong, Japan, Puerto Rico, Singapore na Uingereza Ijumaa ya (September 20).


iPhone5S
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA