Another day, another scandal. Wiki hii Diamond Platnumz ameendelea kutawala vichwa vya habari vya blogs na magazeti ya udaku na kugeuka version ya Tanzania ya Justin Bieber.
Sasha akiwa na mtoto anayedai amezalishwa na Diamond
Wakati ambapo prince huyo wa Bongo Flava hajazijibu tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Dayna pamoja na Baba Levo kuhusu wimbo wake mpya, Number 1, lingine limeibuka tena. Kwa mujibu wa moja ya magazeti ya udaku ya kampuni ya Global Publisher, ameibuka msichana aitwaye Sasha Juma anayedai kuwa amezaa na Diamond.
Msichana huyo anadai alikutana na Diamond Mlimani City jijini Dar es Salaam na akampenda kwakuwa anafanana na mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu. Linasema hawakuchukua muda na wakaanza uhusiano uliowafanya wakutane kimwili na kupelekea msichana huyo kushika ujauzito.
Gazeti hilo linadai Sasha alimpa taarifa staa huyo ambaye alimuomba asitoe mimba kwakuwa atamsomesha msichana huyo aliyefukuzwa shuleni na pia kuahidi kumlea mtoto huyo.
“Ni kweli nimezaa na Diamond. Mtoto ana miezi mitatu sasa. Unajua yeye ndiye alinikatisha masomo na kusema kuwa ataniendeleza na atamlea mtoto hivyo alivyokaa kimya sikuona tena sababu ya kumfuatilia kwa vile kwetu napata kila kitu,” gazeti hilo limemnukuu Sasha.
Limesema lilipomtafuta Diamond kwa simu ambaye kwa sasa yupo nchini Kenya, alijibu: Hahahaaa…mbona hiyo ishu ni kubwa sana kwangu! Ukweli huyo mwanamke simjui kabisa. Lete stori nyingine achana na hiyo.”
Bongo5 imezungumza na mchumba wake Diamond, Penny ambaye amekiri kuisoma taarifa hiyo kwenye mtandao wa Global Publisher na kudai kuwa haijamshtua kwa lolote kwakuwa scandal kama hizo hazimuumizi kichwa na kwamba huja na kupotea.