MAHAKAMA YAKATAA RUFAA YA TAYLOR


130926103655_taylor_liberia_hague_304x171_ap_nocredit_b8f28.jpg
Mahakama maalum ya umoja wa mataifa mjini Hague imekataa ombi la rufaa lililowasilishwa na aliyekuwa Rais waLiberia Charles Taylor baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu wa kivita.
Jaji wa mahakama hiyo amesema kuwa hukumu ya miaka 50 waliompa bwana Taylor kwa kuwasaidia waasi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo ni ya haki.
Bwana Taylor ni rais wa kwanza wa zamani kuwahi kupatikana na hatia katika mahakama ya kimataifa tangu kesi ya Nazi.
Mawakali wake walitaka aachiliwe ,wakidai kuwa kwamba makosa ya kisheria yalifanyika wakati wa kesi yake.
Lakini upande wa mashtaka ulitaka kifungo hicho kuongezwa hadi miaka 80 jela.
Previous Post Next Post