Napenda kutoa Shukrani zangu za dhati kwaMwenyezi Mungu kwa kuweza kunifanikisha
hadi kufikia hapa muda na wakati kama huu...Usiku wa tarehe 29.08.2013 nilikuwa na Launch
video yangu inayotambulika kamaMy Number One,nilianda tafrija fupi kwenyehoteli ya nyota tano,Serena Hotel jijini Dar Es Salaam,ili kuweza kujumuika
na ndugu,jamaa na marafiki wa karibu kuwonesha
kile kitu ambacho nimetumia muda mwingi
kutengeneza,kabla ya kuiachia nikaona vyema
waipitie kabla mtu wangu wa kweli ujaicheki.
Shukrani zangu nyingie ziwaende kwa wageni waalikwa
wote kufika na kutoa support na kushow love kwangu
Sina cha kuwalipa bali kusema asante na mzidi kutegemea
kazi nzuri toka kwangu...
Napenda kuwashukur wasanii wenzangu waliofika
kuangalia video yangu na kuzishukur media zote
na Blogs zote zilizofika kuakikisha wakipata
matukio muhimu kabisa.
Mtu wangu wa kweli unaweza ukache Exclusive Photo kwaajili yako
ujione kilichojiri usiku wa My Number One video Launching
Serena Hotel.
WASAFI......WCB
Picha Picha tu zinahusika sehemu kama hizi.....Kumbukumbu tosha.
William Malecella or U can Call Him Lemutuz.....
I-view Media C.E.O & Founder Raqeey wa kulia na Mpenzi wa Nancy Sumari.
Nancy Sumari,Kulia akiteta jambo na mgeni
mwingeni mwalikwa....Sehemu kama hizi
ukutanisha watu na kubadilishana mawazo...
Kutoka Kushoto A.Y,Shaa,Bench Mark Founder
& EBSS Chief Judge Madam Rita & Salama Jabir
ndani ya nyumba....
Kila mtu Busy na simu kuangalia kianchojiri
kwenye upande wa pili wakisubiria Launching ya
My Number One...
Uncle Salu akukosekana nae,kuhakikisha mambo yanaenda sawa
pembeni ni mama yangu Mzazi BI Sandrah....
Mama Yangu kipenzi akukosekana,Asante
sana mama kwa kufika,Binafsi nafarijika
kuona hata mama yangu mzazi anakubali kazi zangu...
Kelvin Twisa toka VODACOM nae ndani ya Jumba....
Hizi unazoona kwenye Screen ndani ya picha
ni baadhi ya Clip za Behind the scene ya
My Number One....
Babu tale toka Tip Top Connection & Fella toka TMK...
Toka Bongo MOVIE JAY B & RAY walikuwepo kuona
kile ndugu yao wa karibu nini nafanya...
Madee toka Tip Top Connection nae alikuwepo...
Proffesor Jay nae alikuwepo kuakikisha anashuudia
kile ambacho alikuwa akikisikia...
Abdallah au waeza muita Mjukuu wa Ambua basi tumuite Dullah Planet Bongo
ndiye alikuwa anaongoza gurudumu ili kuanzia mwanzo hadi mwisho...
Wenzetu wanaita Master Of Ceremony but
binafsi watu wanaoendesha shuguli yoyote
ya maongezi au Sherehe namuiaga msema Chochote....
Nikitokeza kwa Stage kusalimiana na wageni wangu waalikwa waliofika kwaajili
yangu kushuudia uzinduzi wa Video yangu Mpya.....
Hahaha usiombe usikie nilichoambiwa
hapa mbele....Lazima utatabasamu...
Mama yangu akitabasamu kuonesha ishara ya furaha ndani yake...
Furaha ilioje.....imezidi mpaka imepitiliza...uwiiii
mama yangu nakupenda sana...
SENEDA vipi tena....? Macho Kodoo wapi....
Muda baada ya wadau wangu na watu
wangu wa karibu kuiona video hiyo
hii ilikuwa zawadi yangu kwao,kwa mara ya
kwanza nimetumbuiza my number one
kwenye stage....
Gentleman's.......
Taratibu......
Aghaaa.....Tatu kidonda chako kwangu maradhi......
Kwa mahaba uliyonipa...Nimenogewa.....
Ajajaja Mizuka imepanda....
Woshhhhh.....Balaa sana......
Baada ya kutumbuiza nilikuwa na machache ya kuzungumza nao....
Kutoka Kushoto Sheddy Clever Producer aliefanya My Number one.....
Ommy Dimpoz...Tupogo nae alikuwepogo ndani ya Nyumba.....
G5 CLICK.....
Nikikumbatiana na Ommy Dimpoz...Thanks Man kwa kutokea...
Nilikuwa Busy sana toka nimewasili baada ya
kila kitu ilikuwa time ya kuzunguka na kuongea na kusalimu
wageni waalikwa......Mmoja wapo Kaka yangu
Dully nilienda kusalimiana nae kitambo atujasomana...
Ukikaa na huyu mtu kamwe uwezi nuna pasipo sababu ya msingi.....
Qboy Msafi...Assistance wangu wa karibu...
Nikisikiliza jambo la muhimu toka kwa
Meneja mahusiano wa VODACOM Tanzania...
Dude a.k.a Yahya au waeza mwita Bongo
Dar Es Salaam alikuwepo pia....
Nelly toka G5 Clik ya Clouds Media Group nae ndani...
Ommy Dimpoz & Qboy msafiii
My Blood Rommy Jones au waweza muita Vice
President wa wasafi,Ommy Tupogo,Qboy & Prince Dully
Family....Romeo & Mwengi Ali shem lake....
My Fresh n Blood Sister ESMA KHAN nae
akukosekana licha ya kuwa mbali kidogo lakini
aliweza wahi kuja kunipa support mdogo wake...
Kulikoni Romeo wamfokea Penniel........??? Sielewi
Esma Khan & True Boy Nay....
Kichwa mimi hapa,SALMA msangi & Proffesor J....
Essy & I
Mechoka sana muda huo ilinibidi k
ukimbia kurudi hotelini kupumzika
baada ya siku 4 nyuma kuwa resi muda mwingi
kufanikisha jambo ili,Namshukuru
sana Mungu kwa kufanikisha Jambo ili na Crew
Yangu nzima ya WASAFI CLASSIC BEIBY
Doooh......Noma sana
Memaliza watu wang wa kweli.........