HIizi ndizo Shoo za Ommy Dimpoz Mwisho wa Mwezi huu Marekani


Omary Faraji Nyembo aka Ommy Dimpoz anatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi huu (September) kuelekea nchini Marekani kuanza ziara yake ya muziki katika majiji matatu.
Ommy-2
Hit maker wa ‘Me and You’ Ommy Dimpoz alisaini mkataba wa show hizo toka mwezi (June) na kampuni ya DMK Global Promotion ya mtanzania aishiye Marekani .
Show ya kwanza itafanyika Washington DC Jumamosi (September 21), kabla ya kuelekea Houston Texas kwaajili ya show ya pili (Septermber 28) na kumalizia Los Angeles (October 5). Baada ya show hizo tatu Ommy Dimpoz atarejea Dar es salaam kwaajili ya kumalizia show kubwa ya Serengeti Fiesta.
Ommy-3
DMK Global Promotions ndiyo kampuni iliyowahi kuwapeleka mastaa mbalimbali wa bongo Marekani akiwemo Mr. Nice, Alikiba, Diamond Platnums, Hafsa Kazinja, Khadija Kopa, Linah na sasa ni zamu ya Ommy Dimpoz.
Waandaaji wa ziara hiyo ya Ommy Dimpoz wamefungua website maalum ya www.ommydimpozusa.com kwaajili ya kutoa taarifa za show zake za Marekani ikiwemo kumbi, viingilio nk. hivyo kama na wewe ‘UpoGo’ Marekani usisite kuitembelea.
Previous Post Next Post