Video: Cheni na pete anazovaa Diamond kwa wakati mmoja zinafikia thamani ya shilingi milioni 24


Diamond Platnumz anapenda kuvaa diamonds na Gold.








Akihojiwa juzi kwenye kipindi cha The Trend cha NTV, mtangazaji wa show hiyo Larry Madowo aliuliza thamani ya bling alizokuwa amevaa.
“It’s a bit expensive,” alijibu Diamond huku akizishika bling hizo.
“Kama hii na hii it’s about dola 2000 something au 1,500, hii peke yake dola 2,000.”
Hata hivyo zingine alishindwa kukumbuka bei yake japo kwa kuangalia saa yenye diamond aliyokuwa nayo, pete zingine mbili za dhahabu na almasi na cheni mbili kubwa za dhahabu gharama yake kwa ujumla inaweza kufika dola 15,000 ukijumlisha na hizo zingine alizotaja gharama yake.
“Zina rates tofauti lakini ni gharama kidogo,” alise,a staa huyo.


“Zina ishara? Maanake wengine wanaweza kusema ni Illuminati ama nini,” aliuliza Larry.
“Sidhani mimi navaa tu hii diamond ni jina langu, hii crown as mtu anayelead, kuna diamond nyingi hapa, hii ina alama flani kama ya batman as am flying,” alijibu Diamond.
Aidha Diamond alimtaja Usher Raymond kama msanii anayemtazama na kufuata nyayo zake zaidi.
“I don’t know men, namuona kama anajua sana anachokifanya, tangia nilipokuwa nikimfuatilia mpaka leo. Unajua wanamuziki wengi akitoka mwanamuziki flani yeye anapotea, Usher Raymond yupo. Ukiangalia vitu vyangu mimi namuiba sana.”
Previous Post Next Post