Theo Walcott akifunga bao (HM)
Aaron Ramsey akifunga goli
USHINDI wa mabao 3-1 ambao Arsenal imeupata leo kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Helsinki dhidi ya Manchester City katika mchezo wa kirafiki unamaanisha The Gunners wanaweza kuendelea na maisha bila Luis Suarez.
Arsene Wenger anahaha kusaka saini ya mshambuliaji huyo asiyefurahia maisha Liverpool akiwa ana matumaini makubwa ya kumpata Suarez, licha ya ofa yake ya Pauni Milioni 40 kupigwa chini.
Katika mchezo wa leo, mabao ya Arsenal yamefungwa na Theo Walcott dakika ya tisa, Aaron Ramsey dakika ya 59 na Olivier Giroud dakika ya 62, wakati bao la City limefungwa na Negredo dakika ya 80.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny/Fabianski dk46, Sagna/Jenkinson dk73, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta/Perez dk68, Ramsey/Hayden dk88, Wilshere/Cazorla dk46, Podolski/Giroud dk46, Oxlade-Chamberlain/Zelalem dk74 na Walcott
Manchester City: Hart, Zabaleta (Richards 46), Kompany, Lescott/Boyata dk86, Clichy, Milner/Navas dk46, Fernandinho/Rodwell dk80, Toure/Garcia dk68, Silva, Negredo/Jovetic dk68 na Dzeko/Nasri dk46.
Tags:
Sports