Mwanaume mmoja wa Texas, Marekani aamua kujiondoa uhai akiwa katika wodi ya wazazi saa moja baada ya mke wake kujifungua mtoto wao (August 11).
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi mwanaume huyo Michael Carl Nobles na mkewe Kendra Nobles walisikika wakibishana katika chumba cha hospitali ya Willowbrook Methodist ikiwa ni saa moja toka Kendra ajifungue, kisha Michael alitoa bastola na kujipiga risasi mbele ya mke wake.
Polisi waliendelea kusema wakati wa tukio hilo mtoto aliyezaliwa hakuwa katika chumba hicho na mwanamke huyo hakudhuriwa, Daily mail iliripoti.
Familia ya Michael imesema marehemu alikuwa na matatizo yaliyokuwa yakimpa stress kwa muda kabla ya tukio la kujiua.