Kelele za watu zilinichosha ndo mana nikaamua kwenda kusoma, Adam Haji




Mwigizaji anayefanya vizuri nchini Haji Adam, maarufu kama baba Haji amesema kuwa aliamua kurudi shule kusomea Sanaa na Uigizaji katika chuo cha Sanaa bagamoyo baada ya kuchoshwa na kelele za watu wanaosema kuwa wasanii wa Filamu nchini hawana elimu ya kutosha ndio maana hawafanikiwi katika Uigizaji.
“Nilichoshwa na matusi ambayo kwa kiwango kikubwa yametuandama sisi waigizaji, mara nyingi ilikuwa msanii wa filamu akikosea hata kwa yale mambo binafsi utasikia hao hawajasoma wajinga, sikuwa napenda hivyo katika kuepukana na hilo niliamua kurudi zangu Chuo kwa lengo la kusomea uigizaji na nashukru mungu nimehitimu na kupata Diploma najiandaa kwa ajili ya digrii,” alisema baba haji alipokuwa akizungumza na mtandao wa Filamu central.
Katika chuo hicho alipata nafasi ya kuwa muu wa chuo na anasema kuwa amejifunza mambo mengi sana na amaamini yupo tayari kuipeleka tasnia kwenye viwango vya kimataifa.

Previous Post Next Post

Popular Items