Producer JC wa MZUKA Records Ajipatia Jiko



Producer JC aka Jesus Christ kutoka studio zilizopo Bahari beach dar Es Salaam tanzania na ambae alikua msanii wa tanzania music waliotokaga kipindi hichoo na nyimbo yao iliyokua inajulikana kama “Mpiga Debe”….


Juzi kati amefunga pingu za maisha na mwanadada mwenye asili ya FINLAND huko mjini Arusha na hivi sasa couple hao wameenda mapumzikoni nchini FINLAND kwa muda halafu watarejea nchini kwa ajili ya kuendeleza Fani ya muziki.


Mwanadada huyu ambae nayeye pia ana sikio kubwa sana katika kutengeneza muziki (beats) hii inaonyesha ni jinsi gani Mzuka records itakua imejipanga kwa ujio mpya wa utengenezaji wa muziki wa hapa nyumbani.

Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA