Picha: Simply Madini Tanzania yamzawadia Miss TZ 2012, Brigitte Alfred seti ya vidani vya almasi kwa kujitolea kusaidia jamii..




Kampuni ya Kitanzania ya Simply Madini imemzawadia Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred, seti ya vidani vya almasi kama pongezi kwa jinsi anavyojituma kwenye shughuli za kijamii nchini.


Brigitte akikabidhiwa vidani vya almasi kutoka kwa kampuni ya Simply Madini

Simply Madini hujihusisha na uingizaji wa vidani maridadi vya madini mbalimbali, wakubwa kwa watoto, wanawake pamoja na saa za mkononi kutoka nchini Marekani.


Miss Tanzania 2012 akijaribisha vidani vyake

“Simply Madini imeguswa na miradi ya kusaidia na kurudisha kwa jamii inayofanywa na Miss Tanzania hasa ule wa hivi karibuni wa watoto wenye ulemavu wa ngozi, albino Shinyanga,” imesema kampuni hiyo kwenye maelezo yake.


“As SM we decided to take initiative and award her with one of our finest pieces as a token of appreciation and acknowledgment for her great job. We would like to wish Ms. Brigitte Alfred all the best on the upcoming Miss World Grand Finale next month.”
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA