Serikali ya Kenya imeufunga kwa muda uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA wa jijini Nairobi baada ya kuzuka moto mkubwa kwenye eneo la kufikia na kusababisha shughuli kusimama.
Wafanyakazi wa zima moto wakiendelea na shughuli za kuuzima moto huo
Shughuli za kawaida kwenye uwanja huo wa ndege zinatarajiwa kuendelea baada ya moto huo kuzimwa kabisa.
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka
Rais Uhuru Kenyatta na maafisa wengine wa serikali waliwasili kwenye uwanja huo kuangalia tukio hilo lililoishtua Kenya. Ndege zote zilizokuwa ziwasili leo zimeelekezwa kwenye kutua kwenye viwanja vya ndege vya Mombasa na Eldoret nchini humo.
Moto huo ulianza mida ya saa 10 alfajiri na kwa mujibu wa taarifa za sasa tayari umezimwa.
Hata hivyo chanzo chake bado hakijajulikana.
Serikali imesema wafanyakazi wa zima moto walizidiwa kutokana na kuenea kwa haraka kwa moto huo uwanjani hapo na watu wote wameondolewa kwasababu za kiusalama. Hakuna majeruhi
Tags:
Social