Picha: Peter Okoye wa P-Square amvisha pete ya uchumba mpenzi wake kwa swagger za aina yake



Peter Okoye wa kundi lenye mafanikio makubwa Africa P-Square ameamua ‘personaly’kuzungushia uzio kidole cha mkono wa kushoto wa ‘babies mom’ wake Lola Omotayo kwa style ya aina yake.
Caption: ‘My engagement gift to @Lolaomotayo2011′
Kila mmoja huwa anamaamuzi tofauti ya jinsi ya kumsuprise mpenzi wake wakati wa kutamka jina la uleeeee wimbo wa Rich Mavoko ‘will you marry me’, lakini Star huyo pacha wa Paul Okoye aliamua kumsuprise mpenzi wake wa muda mrefu kwa kumvisha pete ya uchumba (diamond ring), iliyoambatana na gari jipya Range Rover Evoque, maua kuashiria mapenzi, pamoja na ujumbe wa msisitizo ulioandkiwa kwa mkononi uliosomeka “please say YES”.
Hapa aliandika caption: ‘It’s about time….!’
Mpaka hapo naweza kukuachia ubashiri jibu la Omotayo…….
Caption ya picha hii ilikuwa: ‘She said YES….:))’
Na baada ya Peter kupost picha za gari hiyo katika akaunti yake ya Instagram aliongeza na picha ya mkewe mtarajiwa akiwa amevaa pete hiyo ya uchumba na kuandika “Officially Mrs Lola Natasha OKOYE…. Blessed”.
peter
Peter na Lola ni wapenzi wa muda mrefu na wamefanikiwa kupata watoto wawili.
Previous Post Next Post

Popular Items