Rapper Hamidu Chambuso aka Nyandu Tozi, ambaye yupo kwenye maandalizi ya kufanya video ya wimbo wake, Kwa Mafans amesema hali ya muziki ilivyo nchini ilimfanya ajiongezee kufanya mishemishe zingine zinazomweka mjini kwa sasa.
“Kuna wakati nilifanya muziki kama maisha haikuwa kama nilivyotegemea nikaona nifanye misheni town pamoja na ujasiriamali na muziki nifanye kama burudani kwa fans wangu na mimi mwenyewe kwasababu muziki upo kwenye damu,” ameiambia Bongo61. “Kwangu mimi nategemea muziki 30% na zilizobaki nafanya misheni town pamoja na ujasiriamali.”
Rapper huyo amewashauri wasanii ambao muziki hauwaendei vizuri, kuwa wajishughulishe na mambo mengine tofauti.
“Kama muziki umebana usishindane na game utakuwa kichaa fanya muziki kimaslahi kama haulipi fanya mipango mingine na muziki fanya kama burudani,”amesisitiza.