Picha: Majumba Makuu ya Mtaa wa Samora Jijini Dar es salaam Yabomolewa Kupisha Ujenzi wa Barabara Mpya




Ubomoaji wa moja ya majumba kadhaa makukuu katika mtaa wa Samora jijini Dar es salaam umeanza leo jioni na kuendelea hadi usiku kupisha ujenzi wa majumba mapya ambayo hapana shaka yatabadilisha taswira ya mtaa huo ulioanzaa kwa jina la Acacia na baadaye Independence na sasa Samora. Ripota wa zamu katika doria ya sikuu anasema zoezi hilo linaendelea kwa amani na usalama chini ya ulinzi mkali wa polisi


Bomoa bomoa ya majumba ya Samora ikiendelea


Jumba mojawapo likipigwa nyundo


Ni usiku wa saa nne na zoezi linaendelea


Mlinzi akiwa kasimama kidete kuhakikisha zoezi linaendeshwa bila rabsha


Taswira ya eneo la tukio, jirani na iliyokuwa mgahawa wa Salamander ambao nao umeshazungushiwa uzio baada ya kupigwa nyumndo kitambo


Taswira ya mtaa wa Bridge street
Previous Post Next Post